Tunachoamini

Ukiri wa Imani

  1. Mungu ni mmoja wa kweli na aliye katika nafsi tatu milele, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu; na kwamba Yeye ni Roho, asiye ni kikomo, wa milele, asiyebadilika katika pendo Lake, rehema, nguvu, hekima na haki (Isaya 45:22; Zaburi 90:2; Yohana 4:24; 2 Wakorintho 13:14).
  2. Bwana Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu, alikuja katika mwili na kuzaliwa na bikira; kwamba ni Mungu kamili na mwanadamu kamili; kwamba kwa hiari yake alitoa uhai wake kama dhabihu kamili itoshayo kuwa mbadala kwa ajili ya dhambi za mwanadamu; kwamba kwa upatanisho wake mwanadamu atajua uhuru kutoka katika adhabu, hatia na madhara ya dhambi; kwamba alifufuka kutoka kwa wafu katika mwili Wake halisi, mwili wa utukufu, ambao katika huo sasa ameketi Mbinguni, akiwaombea waaminio na kwamba atakuja tena katika mwili wa Wake wa utukufu ili kuanzisha Ufalme Wake. (Mathayo 1:18-25; Yohana 1:14; Wakolosai 1:13-18; 1 Petro 2:24; Luka 24: Waebrania 4:14; Mathayo 25:31-46)
  3. Roho Mtakatifu ni sawa kwa kila hali na Mungu Baba na Mungu Mwana; ndiye aliyetenda muujiza wa kuzaliwa Kristo kama Mwokozi naye anaishi sasa ndani ya waaminio; akiweka mhuri wa siku ya ukombozi; akiwatia nguvu kwa ajili ya huduma; akiwapa karama za neema (karama za roho) kwa ajili ya kujenga mwili wa Kristo (Waefeso 4:30; 1 Wakorintho 6:19, 12:4, 7, 12-13; Matendo 1:5; Tito 3:5)
  4. Kweli ni kamili na halisi. Kweli iokoayo imethibitishwa kwenye Maandiko ya Agano la Kale na Jipya, ambayo ni ufunuo wa Mungu kwa mwanadamu, yaliyotamkwa na kuvuviwa katika asili yake kimaandishi. Biblia ni mamlaka kuu na ya mwisho kwenye masuala yote yahusuyo imani na kutenda. (Mathayo 5:18; 2 Timotheo 3:15-17; 2 Petro 1:20-21)
  5. Kanisa ni mwili wa Kristo uliounganishwa duniani kwa ajili ya ushirika, kujengwa na kwa kupeleka ujumbe wa injili kwa mataifa yote kwa njia ya maisha ya Kikristo na ushuhuda. (Mathayo 28: 19-20; Matendo 1:6-8, 2:41-42; 1 Wakorintho 12:13)
  6. Mwanadamu aliumbwa kwa sura ya Mungu lakini kutokana na dhambi ya Adam alitengwa mbali na Mungu na kuhukumiwa milele. Tiba pekee ya hali hiyo ya mwanadamu ni wokovu kwa mtu mwenyewe kuwa na imani binafsi na katika kazi ya Yesu Kristo. (Yohana 3:15-18; Waefeso 1:7; Warumi 10:9-10)
  7. Kuna ukomo wa uweza kwa viumbe, ikiwa ni pamoja na malaika wasio asi, malaika walio asi na mapepo. Shetani, ni kiongozi wa malaika walio asi; kwa uwazi na dhahiri yeye ametamabulika kuwa adui wa Mungu na mwanadamu, na amehukumiwa kwenda kwenye Ziwa la Moto. (Waebrania 1:4-14, Yuda 6; Mathayo 25:41, Ufunuo 20:10)
  8. Kutakuwepo na ufufuo wa mwili kwa waliookolewa na waliopotea; kwa waliookolewa kwa ajili ya uzima wa milele na kwa waliopotea kwa hukumu ya milele. (1 Wakorintho 15: Danieli 12:1-2; Yohana 5:28-29; 2 Wathesalonike 1:7; Mathayo 5:1-10)